Emine Erdoğan kupewa tuzo na baraza la utu duniani

Mke wa Rais Erdoğan, Emine Erdoğan kukabidhiwa tuzo ya "Changemaker" inayotolewa na baraza la utu duniani

Emine Erdoğan kupewa tuzo na baraza la utu duniani

Mke wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, Emine Erdoğan kukabidhiwa tuzo ijulikanayo kama "Changemaker" yaani mleta mabadiliko. Tuzo hizo hutolewa kwa watu wanaochochea mabadiliko katika jamii zao. Mke huyo wa Rais atakabidhiwa tuzo  kuthamini mchango wake katika kuchochea kazi za kusaidia binadamu. Hafla ya utoaji tuzo hizo itafanyika  jijini London.

Tuzo za "Changemaker"  hutolewa na baraza la Utu duniani na kuzaminiwa na Umoja wa Mataifa ikishirikiana na Uingereza.

Emine Erdoğan, anatarajiwa kukabiziwa tuzo hiyo kati ya tarehe 17-18 April katika hafla maalum ya utoaji tuzo hizo, pia anatarajiwa kuhutubia wageni waalikwa.

 Habari Zinazohusiana