Uturuki yasisitiza kuimarika kwa mahusiano kati yake na Marekani

Uhusiano wa kiuchumi unapaswa kutumika kama njia ya kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Uturuki.

Uturuki yasisitiza kuimarika kwa mahusiano kati yake na Marekani

Uhusiano wa kiuchumi unapaswa kutumika kama njia ya kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Uturuki.

Hayo yamezungumzwa na waziri wa fedha wa Berat Albayrak Uturuki siku ya Jumatatu.

Akizungumzia kwenye mkutano wa viongozi wa biashara katika mji mkuu wa Marekani,Berat Albayrak amesema mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi lazima yawe imara na salama.

Mahusiano ya kiuchumi yanapaswa kuchukua jukumu zaidi katika kuamua uhusiano wa baadaye kati ya nchi hizo mbili.Nafahamu ya kwamba ni  rahisi kuzungumza lakini sio kutekeleza lakini nataka kuwahakikishia ninyi kuwa huu ndiyo mtizamo wetu hii," Albayrak alisema, akikubali kuwa "nguvu za kihistoria na nguvu za taasisi za ushirikiano wa usalama" zimekuwa muhimu katika mahusiano ya nchi mbili.

Albayrak alibainisha matatizo yaliyopo katika mahusiano kati ya washirika wa NATO akisisitiza kuwa ni vyema kutazama yajayo.

"Hebu tujiepushe na vitisho vya vikwazo na michezo ya uharibifu na tufanye kazi katika kujenga ajenda ya kweli" alisema.

Mvutano kati ya Marekani na Uturuki umefikia kiwango kibaya katika miezi ya hivi karibuni na Uturuki sasa imepokea mfumo wa kujihami  wa  S-400 kutoka Urusi,jambo ambalo limepingwa vikali na Washington.Habari Zinazohusiana