Rais wa Uturuki na ujumbe wa maalumu  katika maadhimisho ya ushindi wa Çanakkale

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan atoa ujumbe maalumu katika maadhimisho ya ushindi wa vita vya Çanakkale

Rais wa Uturuki na ujumbe wa maalumu  katika maadhimisho ya ushindi wa Çanakkale


Rais wa Uturuki katika maadhimisho  ya ushindi wa vita vya  Çamakkale na mashujaa amesema kuwa kamwe Uturuki haitorudi nyuma katika  harakti na juhudi zake za uhuru ambazo  Uturuki imeachiwa kama urithi na mababu zake baada ya vita na ushindi wa Çanakkale.

Rais wa Uturuki ametoa ujumbe wake katika maadhimisho ya  miaka 104 ya ushindi wa vita vya Çanakkale kwa kusema kuwa urithi wa mababu waliojitolea kwa hali na mali kuinusuru ardhi ya Uturuki wanastahili heshima kubwa  na  jukumu letu ni kulinda uhuru wetu.

Tunatakiwa kusimama pamoja na  dhidi ya maaduia wanataka kulididimiza  taifa la Uturuki baada ya juhudi kubwa na hatua iliopigwa katika nyanja tofauti.

Bega kwa bega tusimame kidete kuhakikisha  usalama wetu.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar  amezungumza kwa upande wake kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi   wa makundi tofauti kama kundi la PKK/PYG, FETÖ na Deash.
 Habari Zinazohusiana