Rais Erdoğan na Trump waijadili Syria

Rais Erdoğan wa Uturuki na rais Trump wa Marekani wamejadili kuhusu hatua ya Washington kuwaondoa wanajeshi wake nchini Syria.

Rais Erdoğan na Trump waijadili Syria

Rais Erdoğan wa Uturuki na rais Trump wa Marekani wamejadili kuhusu hatua ya Washington kuwaondoa wanajeshi wake nchini Syria.

Kulingana na ikulu ya rais nchinş Uturuki,Viongozi wawili wamekubaliana kuwa uondoaji wa askari wa Marekani kutoka Syria unapaswa kufanywa kulingana na maslahi ya kawaida, akisisitiza haja ya kuunga mkono mchakato wa kisiasa katika nchi iliyoandamwa na vita.

Viongozi hao pia wamegusia uamuzi wao wa kupambana na ugaidi wa aina yoyote.

Pia wamekubaliana kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, kuweka lengo la dola bilioni  75 bilioni katika biashara kati ya nchi mbili.

Kulingana na taarifa ya Ikulu ya Marekani  "White House" Erdogan na Trump wamekubaliana kuendelea kuratibu juu ya kuundwa kwa eneo lenye usalama kaskazini mwa Syria.

Hivi karibuni waziri wa ulinzi wa Uturuki anatarajia kukutana na naibu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan kwa ajili ya mazungumzo zaidi.

Mashambulizi nchini Syria yalianza mnamo mwaka 2011 baada ya serikali ya Bashar al Assad kuwashambulia ghafla waandamanaji nchini humo.

Desemba iliyopita, Trump alitoa tamko la kushangaza ya kwamba Marekani itawaondoa askari wake wote kutoka Syria na kusema kuwa kudi la Daesh limeshindwa nguvu.


Tagi: Syria , Trump , Erdoğan

Habari Zinazohusiana