Taifa, Dharau na Siasa

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

Taifa, Dharau na Siasa

            

Mifumo ya siasa ambayo huendana na jamii pamoja na kukidhi mahitaji ya jamii hiyo huweza kudumu kwa muda mrefu. Mifumo ya siasa inapasa kubadilika kuendana na mahitaji ya jamii, mifumo hiyo inapaswa kuleta faida katika jamii. Mifumo ya siasa ambayo haikidhi mahitaji ya jamii, haiendani na mabadiliko ya jamii, hata iwe imara kiasi gani haitaweza kudumu kwa muda mrefu.

 

Mkuu wa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt, Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anafafanua kuhusiana na mada hii...

 

Katika mtazamo wa kisiasa, tatizo kubwa la mifumo ya kisiasa ya nchi za kiislamu pamoja na zile zisizo za kimagharibi, ni kwamba mifumo hio haikidhi  vya kutosha matakwa ya jamii zao. Mifumo hii ya kisiasa haiakisi vya kutosha mahitaji ya jamii. Baada ya muda aina hii ya mifumo ya siasa huishia kwa kupoteza uhalali wake mbele ya jamii.

Tatizo la pili kubwa na la msingi  la mifumo ya siasa katika nchi zisizo kuwa za kimagharibi ni kuwa mifumo hio haijaandaa mazingira yanayoruhusu mabadiliko ya kiutawala ya kihalali ndani ya mifumo hio. Ni kwa ajili hio utawala wa kisiasa haubadiliki. Uongozi unakuwa wa kudumu.Kwa vile uongozi unaonekana ni wa kihalali miongoni mwa jamii basi mahitajio ya mabadiliko ya uongozi inawezekana yasipewe kipaumbele. Leo hii baadhi ya falme ambazo zinaonekana  halali miongoni mwa jamii zinaweza kuwa mfano mzuri kwa hili. Lakini mifano ya hali hii ni michache sana kiasi tunaweza kusema hakuna. Katika mifano hio hakuna kipimo cha kupima ni kiasi gani watu wanaridhika na utawala wa kisiasa. Ni kwa ajili hio katika dunia ya sasa demokrasia inaweza kuonekana kama kipimo cha uhalali na kuridhika kwa jamii.

Watawala bila wananchi

Mifumo ya siasa inayojumuisha mambo hayo mawili huonekana mifumo bora zaidi. Ile ambayo huacha lolote kati mambo hayo huonekana mifumo mibaya zaidi.Mifumo ya kisiasa ambayo haizingatii mahitaji ya jamii kwa upande mmoja na ile ambayo hairuhusu mabadiliko ya uongozi kwa upande mwingine ni mifumo ambayo huwa na matokeo mbaya kwa jamii.

Mifumo ya siasa inayoonekana imepoteza uhalali wake mbele ya jamii na ile ambayo hairuhusu mabadiliko ya Uongozi inaweza kuonekana sehemu mbalimbali duniani hususani mashariki ya kati. Uongozi wa kisiasa unaokosa uungwaji mkono na wananchi, ambao hauna ridhaa ya wananchi hulazimika kuziba pengo hilo kwa uungwaji mkono na makundi mengine ya kidaraja yake ndani na nje ya nchi. Makundi haya yasiyo ya kidemokrasia ya ndani na nje ya nchi kulingana na maslahi yake, nayo yataendela kuunga mkono na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tawala hizo zinadumu. Nchi nyingi duniani zikiwemo za mashariki ya kati zimeshuhudia tawala za kiimla zikidumu madarakani kwa muda mrefu, na moja wapo ya sababu zilizowezesha tawala hizo  kudumu ni hilo la kuungwa mkono na makundi mengine yasiyo ya kidemokrasia. Vıle aina hii ya utawala hairuhusu mabadiliko ya kihalali ya uongozi, huendelea kuwa mzigo kwa wananchi kwa muda. Aina hii ya utawala hutegemea nguvu za kijeshi na hugeuka kuwa aina ya utawala unaotegemea misaada ya mabeberu kuweza kudumu madarakani.

Udhoefu na mafunzo kutoka Uturuki

Uturuki ambayo imefanya mabadiliko ya mfumo wa kisiasa hivi karibuni inaweza kuwa mfano mzuri utakaosaidia kufafanua tuliyoyaelezea hapo juu. Uturuki ilifanya kura ya maoni na kubadili mfumo wa kisiasa kutoka mfumo wa kibunge kuwa mfumo wa kiurais. Bila shaka zipo nchi duniani ambazo zinatumia vizuri mfumo wa kisiasa wa kibunge. Lakini kwa Uturuki mfumo wa kibunge katika vitendo haukuwa mfumo unaowakilisha uamuzi wa wananchi. Ulibadilika na kuwa mfumo ambao unawakilisha na kujibu matakwa ya makundi ya ndani na nje. Katika kumbukumbu chungu za mfumo huo ni pamoja na vyama vya kisiasa ambayo ilibidi viunganike havikuweza kuonyesha msimamo tofuauti na mkundi ya ndani na nje yaliyowaunga mkono. Vilipaswa kugawana madaraka na makundi hayo.Vile vile kila baada ya miaka10 yalishuhudiwa mapinduzi au jaribiola mapinduzi ya serikali.

Kwa mabadiliko ya mfumo wa kisiasa  iliyoyafanya Uturuki hivi sasa ni vigumu kwa  makundi ya ndani na nje kuingilia uendeshaji wa serikali. Uturuki sasa imekuwa ni nchi ambayo inaweza kujitawala yenyewe bila kuingiliwa. Mfumo wa rais pia umeweka kikomo cha muda wa uongozi kuwa vipindi viwili. Hivyo mfumo wa siasa wa Uturuki unajibu matakwa ya wananchi lakini pia unazingatia na kuruhusu mabadiliko ya uongozi wa kisiasa ( umeweka kanuni za kutosha kuruhusu hilo).Inaweza kusemwa mfumo mpya wa siasa nchini Uturuki umewafanya wananchi kuwa ndio waamuzi wa mwisho.

Ni muhimu sana kwa uongozi wa kisiasa kuwekewa kikomo. Hakuna tatizo lolote ambalo chanzo chake huwa ni kimoja tu. Lakini tukianzia na mashariki ya kati iwapo kanuni hii tu moja ya kikomo cha uongozi ingezingatiwa basi matatizo mengi sana yangekuwa yamepatiwa muafaka. Chukulia mfano kanuni hii ingezikatiwa nchini Syria, utawala wa rais Asad ungekuwa umemalizika muda wake na hilo lingemaliza sehemu kubwa ya matatizo ya Syria.

“Labda kwa lugha kali inaweza kudumu lakini sio kwa dhulma”

Tawala za kiimla Afrika, mashariki ya mbali, na haswa mashariki ya kati hata zionekane zipo  imara au zina nguvu kiasi gani haziwezi kudumu kwa muda mrefu.Hakuna utawala wowote ambao hauzingatii matakwa ya wananchi unaoweza kudumu katika zama hizi za sayansi na teknolojia. Aina hii ya utawala hata uwe na nguvu kiasi gani hata katika historia hazikudumu milele. Leo hii kutoka tawala za “Mongol” na “Crusaders” kimebaki kitu gani? Ni kwa sababu hii miaka elfu moja iliyopita kiliandikwa kitabu cha masuala ya kisiasa na waziri mkuu wa taifa la kuu la Selçuklu Nizamül Mülk “Labda kwa lugha kali inaweza kudumu lakini sio kwa dhulma”

 Katika ufunguzi wa mada hii tuligusia kwamba moja ya tatizo kuu la jamii zisizoza kimagharibi ni kuwa na mifumo ya siasa isiyozingatia matakwa ya wananchi na pia isiyozingatia mabadiliko ya uongozi. Kwa upande wa nchi za magharibi tatizo kuu labda ni kuruhusu vyama vya siasa vilivyokuwa na misingi ya kibaguzi. Kila uchwao vyama vya mrengo wa kibaguzi ndivyo vinavyopewa dhamana ya kuongoza nchi. Ni kwa kiasi gani dunia na Ulaya vipo katika tishio kwa vyama hivi vya kibaguzi kushika madaraka? Majibu ya swali hilo ni mada ya makala nyingine.

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım BeyazıtHabari Zinazohusiana