Putin atoa onyo kali kwa Marekani

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameionya Marekani kuhusiana na makombora ya nchi hiyo barani Ulaya.

Putin atoa onyo kali kwa Marekani

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameionya Marekani kuhusiana na makombora ya nchi hiyo barani Ulaya.

Akizungumza na Bunge la huko Moscow, Putin amesema kuwa kuwepo kwa makombora ya Marekani barani Ulaya - yenye uwezo wa kuipiga Moscow kwa dakika 10 -  ni tishio kwa usalama wa nchi ya Urusi.

Putin ameongeza kwa kusema kuwa Urusi haitokuwa ya kwanza kupeleka makombora yake barani Ulaya lakini hatua kama hiyo kutoka kwa Marekani kutailazimisha Urusi kufanya hivyo hali amabayo itahatarisha usalama wa kimataifa.

"Tunahitaji kuchukua hatua za kutosha katika suala hili",alisema Putin.

"Urusi italazimika kuunda na kupeleka silaha ambazo zinaweza kufikia sio tu maeneo ambayo tutakuwa na tishio nayo moja kwa moja," aliongeza, "lakini pia maeneo ambayo kuna vituo vya kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya mifumo ya makombora inayotishia sisi. "

Putin pia ametangaza maendeleo ya kombora mpya ya hypersonic - Zirkon - yenye uwezo wa kusafiri mara tano kasi ya sauti na ambayo inaweza kufyatuliwa kutoka kwenye nyambizi.

Kuhusu Asia

Putin amezungumzia umuhimu wa mahusiano mazuri kati ya Urusi na nchi barani Asia.

Putin pia ameheshimu mahusiano ya Moscow na nchi za Asia, akielezea mahusiano ya Urusi na China kama "sababu ya kuleta utulivu katika masuala tofauti ulimwenguni" na akaitaja India kama rafiki bora wa kimkakati.

Rais huyo vilevile amegusia mkataba  wa amani kati ya  Urusi na Japan.

"Tuna nia ya kuimarisha ushirikiano wetu na Chama cha Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia," aliongeza Putin .

Moscow, imesema, sasa inasubiri hatua za Umoja wa Ulaya kwa lengo la "kurejesha ushirikiano wa kawaida wa kisiasa na kiuchumi".

Changamoto Muhimu

Putin ameendelea kwa kuelezea mgogoro wa idadi ya watu sasa unaoikabili Urusi kama "changamoto muhimu ya nchi".

Alipendekeza mapendekezo kadhaa ya kutatua mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na kuongeza malipo ya ustawi kwa watoto, msamaha wa kodi, na maboresho katika mfumo wa afya ya umma.Habari Zinazohusiana