Akar ataka ulinzi wa eneo salama ufanywe na Uturuki pekee

Walinzi wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar ataka ulinzi wa eneo salama litakaloundwa mashariki mwa Frati nchini Syria ufanywe na Uturuki

münih güvenlik konferansı.jpg

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar, amesema katika oparesheni za Ngome ya Frati na tawi la mzaituni magaidi wa Daesh zaidi ya laki 3 wameangamizwa. Aliongeza kwamba baada ya jeshi la Marekani kuondolewa nchini Syria, pengo litakaloachwa isiwe ni kwa ajili ya kulifanya eneo hilo sehemu salama kwa magaidi.

Hayo ameyasema katika mkutano wa eneo salama la Munich uliofanyika nchini Ujerumani.

Akar aliseama kwamba rais Erdoğan na rais Trump walizungumza kwa njia ya simu na kufikia muafaka juu ya kuundwa kwa eneo salama nchini Syria.

Akar alisema ulinzi wa eneo hilo salama litakaloundwa kilomita 440 kutoka mpakani mashariki mwa Frati haıtakuwa sahihi wala toshelezi ukifanywa na jeshi la pamoja, kwani eneo salama si kwa ajili ya Uturuki pekee bali hata kwa wananchi wa Syria walio ukimbizini watakapokuwa wakirejea makwao. Akar alisema ulinzi wa eneo hilo unpaswa kufanywa na Uturki pekee.

 Habari Zinazohusiana