YTB yaendelea kutoa udhamini wa masomo nchini Uturuki

Kiongozi wa YTB Abdullah Eren amesema kuwa idadi ya wanafunzi wa kigeni nchini Uturuki inatarajia kuongezeka kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia mwaka 2020.

Uturuki ina lengo la kufikisha zaidi ya wanafunzi 200,000 wanaodhaminiwa katika masomo yao mpaka kufikia mwaka 2020.

Katika miaka ya 2000 Uturuki ni moja ya nchi ambazo zilikuwa na shughuli nyingi sana katika siasa za nje. Moja ya faida ya shughuli hizo ni kuongezeka kwa idadi ya waturuki wanoishi nje ya Uturuki ambao hivi sasa idadi yao ni zaidi ya milioni 6.

Mwaka 2010 ilianzishwa kurugenzi ya waturuki pamoja na jamii ndugu waishio nje ya nchi (YTB). Kurugenzi hii kazi yake ilikuwa ni kubuni sera na kusimamia utekelezaji wa sera hizo.

Kurugenzi hii ya YTB ilifanya kazi kama taasisi ya kidiplomasia kwa wanadiaspora wa Kituruki ( waturuki waishio ughaibuni),  Katika  kuraisisha michakato na shughuli za waturuki waishio nje  hasa bara la Ulaya, sambamba na hilo shughuli nyingine ni kulinda na kuendeleza utambulisho wa kiutamaduni kwa watuturki waishio ughaibuni.

 Habari Zinazohusiana