Wafanyakazi wa viwanja vya ndege nchini Ujerumani kugoma

Kutokana na mgomo uliopangwa kufanyika hapo kesho katika viwanja vya vya ndege mjini Berlin baadhi ya safari zitacheleweshwa na zingine zitafutwa

Wafanyakazi wa viwanja vya ndege  nchini Ujerumani kugoma

Kutakuwa na mgomo wa wafanyakazi katika viwanja vya ndege viwili mjini Berlin nchini Ujerumani siku ya Jumatatu.

Kuchelewa na kufutwa kwa baadhi ya safari za ndege katika viwanja hivyo ndio mambo yanayogonga vichwa vya habari hivi sasa,kutokana na onyo la mgomo lilitolewa na jumuiya ya wafanyakazi wa vitengo vya usalama kabla hawajafanya mazungumzo ya kujadili maslahi  na marupurupu yao.

Mgomo huo utakuwa katika viwanja vya ndege vya Tegel na Schönefeld vya mjini Berlin nchini Ujerumani, na utafanyika siku ya Jumatatu kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 3 asubuhi kwa masaa ya nchi hiyo.

Wafanyakazi hao wapatao elfu 23 watafanya mgomo huo kabla hawajafanya kikao cha majadiliano kuhusiana na marupurupu na mishahara yao. Mgomo huo ni kwa ajili ya kuwekea msisitizo mahitajio yawe yachukuliwe kwa uzito wake.

Waajiri walipendekeza kwamba waongeze mishahara ya wafanyakazi mara moja kwa kila miaka miwili kwa kiwango cha asilimia 1.8 mpaka asilimia 2.

Jumuiya ya wafanyakazi kwa upande wao ilipendekeza wafanyakaziwanaofanya kazi katika vitengo vya mizigo na abiria mishahara yao iongezwe kutoka Euro 17 kwa saa moja mpaka Euro 20 kwa saa.

Mkutano wa majadiliano baina ya waajiri najumuiya ya wafanyakazi unatarajiwa kufanyika Januari 23.  

 

 


Tagi: Ujerumani

Habari Zinazohusiana