Maafisa kutoka Saudia walilipia vyumba 500 katika hoteli za Trump nchini Marekani

Mwaka 2016 maafisa kutoka Saudia walioenda kufanya ushawishi "lobbying" kwa serikali mpya ya Marekani walilipia gharama ya miezi 3 vymba 500 kwenye hoteli za Trump

Maafisa kutoka Saudia walilipia vyumba 500 katika hoteli za Trump nchini Marekani

Kwa mujibu wa jarida la Washington post, limefahamisha kwamba mwaka 2016 mara tu baada y uchaguzi mkuu wa rais maafisa kutoka Saudia ambao walikwenda kufanya ushawishi kwa serikali mpya kwa niaba ya serikali ya Saudia, walilipia karibu vyumba 500 gharama ya miezi 3 mfululizo katika hoteli ya rais Donald Trump iliopo jijini Washington. 

Kwa mujibu wa nyaraka zilizofikiwa na jarida hilo la Washington post,  wawakilishi hao waliotumwa kufanya ushawishi na serikali ya Saudia walipia hoteli hiyo ambayo mpaka sasa inamilikiwa na rais huyo wa marekani dola za kimarekani 270,000.

Habari hio inaendelea kusema kwamba  kuanzia mwaka 2017 mapaka hivi sasa wateja kutoka Saudia ambao walikaa katika hoteli za Trump za Chicago na mjini New York imeongezeka, vile vile wageni walioambatana na mwana mfalme Muhammed bin Salman walifikia hoteli ya Trump ya jijini New York. Faida za hoteli hizo zimeongezeka kwa asilimia 25.

 Habari Zinazohusiana