Rais mpya wa Mexiko atangaza kuuza ndege ya kifahari ya rais anayemaliza muda wake

Mexiko imetangaza kuuza ndege 60 na helikopta 70 zilizokuwa zikitumiwa kwa matumizi ya serikali ikiwamo ndege ya kifahari ya rais wa anayemaliza muda wake

meksika eski dv.bşk.nın ucagi1.jpg

 

Ndege ya kifahari ya rais wa zamani wa Mexiko kuuzwa.

Rais mpya wa Mexiko aliyeapa na kuanza kutumikia wazifa huo Decemba 1, Andres Manuel Lopez Obrador ameanza kazi kwa kutangaza kuiuza ndege ya kifahari ya rais wa zamani.

Obrador amesema watauza ndege na helikopta walizokuwa wanatumia wanasiasa wala rushwa.

Baada ya maelezo hayo ya Obrador waziri wa fedha wa nchi hiyo, Carlos Urzua akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari alisema kwamba hivi karibuni tangazo rasmi la kuuza ndege hiyo aina ya Boeing 787 Dreamliner litatolewa. 

Waandishi wa habari waliruhusiwa kupiga picha ndani ya ndege hiyo ya rais  anayemaliza muda wake, ambako ilionekana bafu la ndege hiyo limesakafiwa kwa mawe ya thamani ya marumaru.

Waziri Urzua alisema ndege hiyo iliyonunuliwa mwishoni mwa mwaka 2012 kwa thamani ya dola za kimarekani milioni 218, pamoja na ndege zingine 60 na helikopta 70 za serikali zitauzwa.

Obrador wakati wa kampeni aliahidi akishinda atauza ndege zote za kifahari za wizara mbalimbali za serikali. rais alisema kwa atakaye nunua ndege hizo yeye mwenyewe ataenda kumkabidhi ndege katika sherehe rasmi ya makabiziano.

Katika maelezo mengine Obrador alisema inatia aibu sana kwa umaskini uliokithiri katika nchi hio kuendelea kuwa na ndege za kifahari kwa ajili ya viongozi, alisema atashindwa kumuangalia mtu yeyote usoni ikitokea akatumia ndege hizo.

 


Tagi: Mexiko , Obrador

Habari Zinazohusiana