Nikki Haley : "Urusi na Iran zaweka kipingamiza katika pendekezo la Uturuki kuhusu Idlib"

Maukilishi wa Marekani  Umoja wa Mataifa Nikki Haley amezungumzia pendekezo la Uturuki  kusitishwa mapigano Idlib na mwenendo wa Urusi na Iran

Nikki Haley : "Urusi na Iran zaweka kipingamiza katika pendekezo la Uturuki kuhusu Idlib"

Muakilishi wa Marekani Nikki Haley  katika mkutano wa baraza la usalama uliofanyika kwa ajili ya Idlib Jumanne amesema kuwa Uturuki inahitaji  kusitishwa kwa mapigano huku Urusi na Iran zikipinga pendekezo hilo.

Mkutano huo wa baraza la usalama umefanyika baada  ya mkutano uliofanyika mjini Tehran kati ya Uturuki, Urusi na Iran.

Nikki Haley amesema kuwa Urusi na Iran  hazioneshi  ushirikiano katika juhudi za kisiasa za  kutatua mgogoro wa Syria.

Nikki Haley ameendelea kusema kuwa hatua zozote  Idlib  ni kutokana na  nyendo za Iran na utawala wa Syria .

Muakilishi wa Marekani ameendelea akisema kuwa  Marekani haitokubalia  Urusi kuendelea kuharibu mazungumzo ya kisiasa  kuhusu Syria huku ikifahamu vema kuwa Assad hatilii maanani  mazungumzo na wakati huo huo Urusi inaendelea kushambulia Syria na kusababisha hasara.

Mashambulizi dhidi ya Idlib yanatakiwa kusitishwa na misaada ya kibinadamu  kuhurusiwa kuingia katika maeneo  yanayohitaji msaada.

Kwa upande wake muakilishi wa Urusi Umoja wa Mataifa  Vassili Nebenzia  ametupilia mbali tuhuma zilizotolewa na Haley dhidi ya Urusi kwa kusema kuwa Syria ni taifa huru.

 

 Habari Zinazohusiana