Mke wa rais wa Uturuki apewa tuzo na Baraza la wafadhili la kiislamu ulimwenguni

Mke wa rais wa Uturuki Bi Emine Erdoğan amepewa tuzo na baraza la wafadhili la kiislamu ulimwenguni mjini London

Emine E.jpg
Emine.jpg

Bi Emine Erdoğan, mke wa rais wa Uturuki amepewa tuzo na  baraza la  wafadhili la kiislamu ulimwenguni katika hafla ilioandaliwa mjini London  Jumatatu nchini Uingereza.

Bi Emine Erdoğan amepewa tuzo hiyo kwa mchango wake  mkubwa katika juhudi za kutoa misaada kwa watu wanaohitaji misaada ulimwenguni.

Mke wa rais wa Uturuki amepokea tuzo hiyo akisema kuwa Uturuki ni taifa  ambalo huwakumbuka watu ambao wanahitaji misaada katika  maeneo tofauti ulimwenguni.

Emine Erdoğan ametoa shukrani  baada ya kupewa tuzo hiyo  kupitia ukurasa wake wa Twitter na Facebook.

 Habari Zinazohusiana