Mvutano kati ya Marekani na Uturuki

Mvutano kati ya Marekani na Uturuki

Mvutano kati ya Marekani na Uturuki

 Mvutano kati ya Marekani na Uturuki umeshuhudiwa kupamba moto katika siku chache zilizopita. Mvutano huo umeshuhudiwa katika ya mataifa mawili wanachama wa muungano wa jeshi la kujhami la Magharibi NATO.

Hali ya ushirikiano katika muungano huo tangu mwaka 1952 ilikuwa ikijadiliwa kwa muda mrefu. Sera za nje za Uturuki haswa katika utawala wa chama cha AKP ni kwamba Uturuki ilinde maslahi yake katika ukanda, inafahamika kuwa katika ukanda Marekani ilikuwa na ushawishi mkubwa.

 Kutokana na  kufuatiliwa  kwa kiongozi wa kundi la wahaini wa FETÖ Fetullah Gülen ambae amepewa hifadhi nchini Marekani na kuishi kwa  amani Pennsylvania, jambo hilo limepelekea ushirikiano katika ya Marekani na Uturuki kuwa  katika hali ya mvutano. 

Vile vile hali ya mvutano kati ya Marekani na Uturuki imezidi kuongezeka kutokana na Marekani kutoa usaidizi kwa kundi la kigaidi la YPG ambalo linafahamika vema kuwa tawi la kundi la kigaidi la PKK nchini Syria. Marekani imefahamisha ya kwamba kundi hilo ni mshirika latika kukabiliana na makundi ya kşgaid katika ukanda. Wakati huo huo Uturuki inafahamisha ya kwamba hatua hiyo na uamuzi wa Marekani kushirikiana na kundi kama hilo ni jambo lisilokubalika hata mara moja.

Inafahamika vema ni kiasi gani  uwepo wa kundi la PKK katika  mipaka ya Uturuki  ni hatari kwa usalama wa Uturuki na ni tishio  kwa Uturuki. Tukiweka kando mvutano huo , kumezuka mvutano mwingine ambao umesababishwa na kukamatwa kwa mchungaji Brunson wa Marekani na mfumo wa kujihami na makombora wa S-400 ambao Uturuki imenunua kutoka Urusi.

Uturuki imenunue mfumo huo kwa ajili ya kujihamai na makombora  kama ilivyo wajibu wa taifa lolote  kulinda mipaka yake.

Kukamatwa kwa Brunson na mfumo wa S-400 vimepelekea pia hali ya vuta ni kuvute kati ya Marekani na Uturuki.

 Baraza la seneti lilitaka Brunson aachwe huru.  Rais wa Marekani Donald Trump amelazimisha  kuachwa na mchungaji huyo wakati wa mazungumzo na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan.  Rais wa Marekani alitoa ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akilazimisha kwa vitisho kuachwa huru kwa  mchungaji huyo aliekamatwa Brunson.  Brunson alikamatwa kwa akituhumiwa kushirikiana na wanamagmbo wa kundi la PKK  , kundi ambalo linafahamika kuwa kundi la kigaidi na wahaini wa kundi la FETÖ ambalo wanachama wake wanatambulika vema katika jaribio la mapinduzi Julai 15.

Kwa lengo la kujipatia wapiga kura kutoka katika kundi la  wainjilisti Marekani makamu wa rais wa Marekani Mike Pence  alitoa vitisho  dhidi ya Uturuki akilazimisha  mchungaji Brunson aachwe huru. Vitisho vya vikwazo dhidi ya Uturuki vilitolewa na Marekani kupitia makamu wake wa rais. Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu  alisema kwa upande kuwa Marekani  inatakiwa kuheshimu uamuzi wa  mahakama ya Uturuki  na sio kuitolea vitisho Uturuki.

Vita vya kiuchumi kati ya Uturuki na Marekani baada ya uamuzi wa Marekani kuiwekea vikwazo Uturuki ilianza. Soko la fedha na thamani ya sarafu ya Uturuki ilianza kushuka thamani yake. Kwa muda wa siku mbili sarafu ya marekani iliweza kupata wakatia mbapo sarafu ya Uturuki ilionekana kupoteza thamani yake. 

Mamlaka husika nchini Uturuki ilikabilana na  hali hiyo  hadi kuhakikisha kuwa sarafu ya Uturuki inarejea katika thamani yake ya hapo awali.

Sarafu ya Marekani katika soko la fedha Uturuki ilifikia thamani ya Lira 7 na kushuka hadi 6 kwa muda wa siku kadhaa.

Wakati huo huo waziri wa fedha  Berat Albayrak  alifahamisha kuanza kwa mfumo mpya katika uchumi wa Uturuki. Kukisubiriwa  mfumo mpya huo katika  sekta ya uchumi Uturuki, rais wa Marekani Donald Trump  baada ya kuiewekea vikwazo Uturuki katka bidhaa za chuma  ameendelea kutuhumu ukukwaji wa haki na vitendo vya unyanyasaji.

Licha ya thumu hizo kuathiri thamani ya sarafu ya Uturuki, sarafu ya Uturuki ileweza kujimuda na linda thamani yake dhidi ya sarafu ya Marekani. Wkati huo Marekani ikijaribu kuudoofisha uchumi wa Uturuki , Trump anaishambulia China kaztika sekta yake ya uchumi.

Kufuatia mashambulizi  hayo ya rais wa Marekani dhidi ya  sekta ya uchumi Uturuki, China, Urusi na China pia zimeafikiana  kutumia sarafu ya ndani katika biashara  baina ya  mataifa hayo. Baada ya Marekani kushambulia Uturuki katika sekta yake ya uchumi,  Urusi na Iran vimeonesha wazi kuwa pamoja na Uturuki katika kukabiliana na jambo hilo ambalo lengo lake ni kudhoofisha  uchumi wa Uturuki.

Umoja wa Ulaya pia iunaathirika na vikwazo vya Trump dhidi ya Uturuki kwa  baadhi ya mashirika y kutoka katika mataifa ya umoja huo yamewekeza nchini Uturuki.

Ujerumani imeonesha ushirikiana na Uturuki suala hilo, Uhispania na  Italia pia zilionesha ushirikiano.Habari Zinazohusiana