Balozi wa Uturuki mjini Washington afanya mkutano na baraza la usalama la Marekani

Balozi wa Uturuki mjini Washington Serdar Kılıç afanya  mazungumzo na baraza la usalama la Marekani

Balozi wa Uturuki mjini Washington afanya mkutano na  baraza la usalama la Marekani

 

Balozi wa Uturuki mjini Washington Serdar Kılıç afanya mazungumzo na baraza la usalama la Marekani White  House  na kuzungumzia suala zima kuhusu kukamatwa kwa  mchungaji wa Marekani  na vyombo vya usalama nchini Uturuki.

Balozi Serdar Kılıç amesema kuwa mchungaji huyo alikamatwa  akituhumiwa  kushirikiana na  kundi la wahaini wa FETÖ na wanamgambo wa kundi la kigaidi la PKK.

Serdar Kılıç amekutana pia  na mshauri wa  usalama wa mataifa  John Bolton White  House .

Msemaji wa ikulu  White House Sarah Sanders ametoa taarifa kuhusu mkutano huo.

Taarifa zimefahamisha kuwa  mazungumzo baina ya viongozi hao  yaligubikwa na  suala zima la ushirikiano kati  ya Marekani na  Uturuki ikiwemo pia mchungaji  aliekamatwa.

 

 Habari Zinazohusiana