Idadi ya vifo kutokana na tetemeko yaongezeka nchini Indonesia

Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi lililtokea Loloan nchini Indonesia katika umbali wa kilomita 10,5 Mashariki-Kusini mwa eneo hilo imezidi kuongezeka na kufikia watu 105.

1027750

Tetemeko hilo ambalo lilikuwa na ukubwa wa 7,0 katika kipimo cha Rishter limesababisha uharibifu na maafa makubwa katika eneo hilo.

Tetemeko hilo limetokea  katika  kisiwa cha Lombok ambacho hutuembelewa kwa wingi na watalii.

Ni mara ya pili kwa eneo hilo kukumbwa na tetemeko la ardhi.

 Mnamo Julia 29 watu 16 walifariki na majumba kadhaa kubomoka kutokana na tetemeko.

Maeneo tofauti  yamekumbwa na ukosefu wa umeme, madaraja yamebomoka  na kupelekea shughuli za uokoaji kuwa ngumu zaidi.Habari Zinazohusiana