Shambulizi la kujitoa muhanga lasababisha vifo vya watu wanne Afghanistan

Shambulizi la kujitoa muhanga limesababisha vifo vya watu wanne katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan.

1020271
Shambulizi la kujitoa muhanga lasababisha vifo vya watu wanne Afghanistan

Shambulizi la kujitoa muhanga limesababisha vifo vya watu wanne katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan.

Msemaji wa polisi Hashmat Stanikzey amesema kuwa bomu hilo limelipuka karibu na wilaya ya Kampani.

Watu wanne wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine sita wakiwa wamejeruhiwa.

Walioshuhudia shambulizi hilo wamesema kuwa watu watano wamepoteza maisha.

Kundi la Taliban limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana