Idadi ya vifo kutokana na mafuriko yafikia 222 Japan

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mafuriko kwa sasa imefikia 222 nchini Japan.

1014996
Idadi ya vifo kutokana na mafuriko yafikia 222 Japan

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mafuriko kwa sasa imefikia 222 nchini Japan.

Mvua kali zilizoambatana na upepo kali zilinyesha Magharibi mwa Japan na kusababisha maafa hayo ambayo idadi yake inazidi kuongezeka.

Habari zimefahamisha kuwa huenda idadi hiyo ikazidi kuongezeka kwa kuwa watu wasiopungua 60 bado hawajulikani walipo.

Watu zaidi ya 700 000 wanaendesha  shughuli za kuwatafuta watu ambao hawajulikani walipo.

Maeneo ambayo yameathirika kwa kiasi kikbwa na mafuriki ni pamoja na eneo la Hiroshima, Okayama na Ehime.

Watu zaidi ya 6 700 hawana makaazi kutokana na mafurikoHabari Zinazohusiana