Idadi ya vifo kutokana na mafuriko yaongezeka nchini Japan

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko yaliotkea nchini Japani yaongezeka na kufikia watu 209.

1012321
Idadi ya vifo kutokana na mafuriko yaongezeka nchini Japan

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko yaliotkea nchini Japani yaongezeka na kufikia watu 209.

Taarifa kuhusu idadi ya maafa kuongezeka imetolewa na  kituo cha habari cha Kyodo cha nchini Japan.

Mvua kali zilizoambatana na upepo kali zilinyesha Magharibi mwa Japani na kusababisha maafa hayo ambayo idadi yake inazidi kuongezeka.

Kituo hicho cha  habari kimefahamisha kuwa huenda idadi hiyo ikazidi kuongezeka kwa kuwa watu wasiopungua 60 bado hawajulikani walipo.

Watu zaidi ya 700 000 wanaendesha  shughuli za kuwatafuta watu ambao hawajulikani walipo.

Maeneo ambayo yameathirika kwa kiasi kikbwa na mafuriki ni pamoja na eneo la Hiroshima, Okayama na Ehime.

Watu zaidi ya 6 700 hawana makaazi kutokana na mafuriko.Habari Zinazohusiana