Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko nchini Japani yazidi kuongezeka

Idadi ya watu waliofariki katika mafuriko yaliotokea nchini Japani yaongezeka na kufikia watu 195

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko nchini Japani yazidi kuongezeka

 

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko yaliotkea nchini Japani yaongezeka na kufikia watu 195. Taarifa kuhusu idadi ya maafa kuongezeka imetolewa na  kituo cha habari cha Kyodo cha nchini Japani.

Mvua kali zilizoambatana na upepo kali zilinyesha Magharibi mwa Japani na kusababisha maafa hayo ambayo idadi yake inazidi kuongezeka.

Kituo hicho cha  habari kimefahamisha kuwa huenda idadi hiyo ikazidi kuongezeka kwa kuwa watu wasiopungua 60 bado hawajulikani walipo.

Watu zaidi ya 700 000 wanaendesha  shuhuli za kuwatafuta watu ambao hawajulikani walipo. Maeneo ambayo yameathirika kwa kiasi kikbwa na mafuriki ni pamoja na eneo la Hiroshima, Okayama na Ehime.

Watu zaidi ya 6 700 hawana makaazi kutokana na mafuriko.

 Habari Zinazohusiana