Uturuki yaongoza ulimwenguni kwa kutoa misaada ya kiutu

Uturuki yaorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwa kutoa misaada ya kiutu ulimwenguni

Uturuki yaongoza  ulimwenguni kwa kutoa misaada ya kiutu

Uturuki yashika nafasi ya kwanza kwa kutoa  misaada ya kiutu ulimwenguni  na shirika la  maendeleo la kujitolea  la nchini Uingereza. Shirika hilo katika ripoti yake limesema kuwa Uturuki mwaka 2017 imeshika nafasi ya kwanza kmwa kutoa misaada ya kiutu  kwa thamani ya dola bilioni 8,07.

Uturuki ni taifa ambalo limetoa kiwango kikubwa cha misaada ya kiutu ulimwenguni mwaka 2017.

Katika orodha hiyo iliotolewa na ripoti ya shirika hilo la Uingereza, Uturuki inaongoza ikifuatwa nyuma na Marekani, Ujerumani na Uingereza.

Mashirika ya  Umoja wa Ulaya yamechukuwa nafasi ya 4 na gharama ya thamani ya dola bilioni 2,2.

 


Tagi: İHH , AFAD , misaada , Uturuki

Habari Zinazohusiana