Korea Kaskazini kufunga kituo chake cha majaribio la makombora yake ya nyuklia

Hafla ya kufunga kituo cha majaribio cha makombora ya nyuklia Korea Kaskazini itafanyika kati ya Mei 23 na Mei 25 mwaka 2018

969452
Korea Kaskazini kufunga kituo chake cha majaribio la makombora yake ya nyuklia

Korea Kaskazini imeweka bayana Jumamosi kuwa itafunga kituo chake cha majaribio cha makombora ya nyuklia . 

Kituo cha habari cha Yonhap cha Korea Kaskazini kimenukuu taarifa zilizotolewa na wizara ya mambo ya  nje ya Korea Kaskazini kuwa zoezi la kiufundi la kuanza  kufunga kituo cha majaribio  ya makombora ya nyuklia  tayari limepangwa kuanza ifikapo Mei 23.

Kituo cha  majaribio ya makombora cha Pyunggye-ri  kinachopatikana Kaskazini Mashariki mwa Korea  kitafungwa.

 Habari Zinazohusiana