Uturuki na Ujerumani zaahidi kuimarisha mahusiano yao

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wameahidi kuimarisha mahusiano kati ya nchi zao baada ya kuwa katika migogoro kati ya Ankara na Berlin miezi kadhaa iliyopita

Uturuki na Ujerumani zaahidi kuimarisha mahusiano yao

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wameahidi kuimarisha mahusiano kati ya nchi zao baada ya kuwa katika migogoro kati ya Ankara na Berlin miezi kadhaa iliyopita.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin ,Yıldırım amesisitiza ushirikiano katika kupambana na ugaidi.

Waziri Yıldırım amenukuliwa akisema,"PKK ni kundi la kigaidi.PYD/YPG ni kundi la kigaidi pia.YPG ni tawi la PYD/PKK na suala hili limethibitishwa na Uingereza pamoja na Marekani.Haijalishi wanajiita majina gani,wote wana ajenda ileile ya kuvuruga amani na kuzua migogoro."

Uturuki imetaka Ujerumani iliunge mkono suala hilo.

Merkel naye amesema anaamini mkutano huo utasaidia kuimarisha uhusiano baina yao.

Hata hivyo Merkel amesema kuwa kuna ugumu fulani  katika suala zima la mahusiano kati ya nchi hizo mbili na hivyo basi ni vyema mazungumzo ya kina yaendelee kufanywa.

 

 

 Habari Zinazohusiana