Kituo cha utamaduni cha kiislamu chashambuliwa Poland

Kituo cha utamaduni cha kiislamu chashambuliwa  mjini Varsovia nchini Poland

856433
Kituo cha utamaduni cha kiislamu chashambuliwa Poland

 

Msemaji wa jeshi la Polisi mjini Varsovia  Mariusz Mrozek amesema kuwa  madirisha ya kituo cha utamaduni wa kiislamu mjini humo  yamevunjwa na watu ambao bado hawajajulikana.

Kituo hicho cha  utamaduni  kinajumuisha jengo la mskiti,   chumba cha mikutano, maduka na mgahawa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Poland, viongozi wa dini ya uislamu watafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo.

Mandamano pia yanatarajiwa kufanyika  kusini mwa Poland.

Polisi mjini Varsovia imefahamisha kuwa imeaanzisha uchunguzi ili kuwatia nguvuni waliohusika na kitendo hicho cha uharibifu.

Katika  siku za chache zilizopita nchini Poland kumeripotiwa vitando vinavyo ashiria chuki dhidi ya wageni.Habari Zinazohusiana