Mwanamume avamia duka na kuua mmoja Ujerumani

Mwanamume mmoja ameripotiwa kuvamia duka kubwa "supermarket" na kumchoma mwanamume mmoja kisu wakati watu wakihemea vitu mjini Hamburg nchini Ujerumani

779892
Mwanamume avamia duka na kuua mmoja Ujerumani

Mwanamume mmoja ameripotiwa kuvamia duka kubwa "supermarket" na kumchoma mwanamume mmoja kisu wakati watu wakihemea vitu mjini Hamburg nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa habari,mtu huyo aliyechomwa kisu alifariki papo hapo huku wengine 6  wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Mwanamume huyo alikamatwa na polisi pale alipotaka kukimbia.Raia wa Uturuki mwenye umri wa miaka 35 ameripotiwa kusaidia katika kumkamata mshambuliaji huyo.

.Polisi wanaamini kuwa mshambuliaji huyo ni raia wa Emirates mwenye umri wa miaka 26.

Hata hivyo uchunguzi zaidi kuhusu shambulizi hilo unazidi kufanyika.Habari Zinazohusiana