Waziri wwa utamaduni wa Uturuki afanya ziara Palestina Nabi Avcı

Waziri wa utalii na utamaduni wa Uturuki akutana na waziri wa utamaduni na utalii wa Palestina

668326
Waziri wwa utamaduni wa Uturuki afanya ziara Palestina Nabi Avcı

 Waziri wa utamaduni na utalii wa Uturuki Nabi Avcı afanya ziara Palestina na kufanya mazungumzo na waziri wa utamaduni na utalii wa Palestina.

Baada ya kufanya ziara yake rasmi Israel waziri  Nabi Avcı alijielekeza Palestina.

Waziri wa utamaduni na utalii wa Uturuki alikutana na waziri wa utamaduni na utalii wa Palestina Ehad Bessairo mjini Ramallah  ambapo walizungumzia kuhusu ushirikiano na msaada wa Uturuki kwa Palestina.

Viongozi hao walifahamisha kuwa mkutano wao huo ulihusu ushirikiano katika sekta tofauti na ushirikiano.

Baada ya kumaliza mkutano wao viongozi hao walitia saini kuhusu makubaliano ya ushirikiano katika utamaduni.

Waziri Nabi alfanya ziara pia katika kaburi la kiongozi wa mamlaka ya wapalestina Yasser Arafat.Habari Zinazohusiana