Tamasha la utamaduni wa Kituruki nchini Marekani

Tamasha la 14 la utamaduni wa Kituruki liliandaliwa katika mji wa Washington nchini Marekani

576853
Tamasha la utamaduni wa Kituruki nchini Marekani

Tamasha la 14 la utamaduni wa Kituruki liliandaliwa katika mji wa Washington nchini Marekani.

Wananchi wengi wa Kituruki pamoja na raia wengine wanaoishi Marekani walihudhuria tamasha hilo lililoshirikisha chama cha ATA-DC cha Waturuki na Wamarekani. 

Tamasha hilo lilifana na kuvutia wengi kwa aina mbalimbali za vyakula vya utamaduni wa Kituruki na maonyesho ya densi za kiasili.

Washiriki pia walipata fursa ya kutambulisha vyombo vya kiasili vilivyokuwa vikitumika kipindi cha utawala wa Ottoman kama vile mazuliana, samani za nyumba na vyombo vya kaure.

Mavazi ya kipekee ya utamaduni wa Kituruki pamoja na miundo ya kisanii pia vilikuwa miongoni mwa vivutio kwenye tamasha hilo.

Wakati huo huo, michezo mbalimbali ya watoto waliohudhuria na familia zao pia lilikuwepo. Habari Zinazohusiana