Waziri Orban : « Wakimbizi watishia utamaduni wa kikristuo»

Mamia ya wakimbizi waliokuwa wakisubiri kwa muda wa siku kadhaa Budapest wamesafirishwa kwa mabasi

374760
Waziri Orban : « Wakimbizi watishia utamaduni wa kikristuo»

Baada ya kufunguliwa kwa kituo cha treni kilichokuwa kimefungwa kwa muda wa siku mbili Hungari ambapo hali ya msongamano iliokuwa imesababishwa na idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Syria ilikuwa ikiripotiwa Ujerumani na Austria zafahamisha kuwa zitawapokia baadhi ya wakimbizi wanaoomba hifadhi.

Waziri mkuu Viktor Orban anaepinga kupewa hifadhi wakimbizi hao alifahamisha kuwa hakuna mkimbizi atakaeondoka Hungary bila ya kusajiliwa.

Mkataba kuhusu wakimbizi barani Ulaya unafahamisha kuwa mkimbizi husajiliwa katika ardhi ya kwanza atakayofikia pindi anapoingia Ulaya kwa mara ya kwanza.Wakimbizi walioko Hungary wanaotaraji kuingia Ujerumani wanakata kusajiliwa nchini humo.

Orban katika mkutano na waandishi wa habari akishirikiana na spika wa bunge la Ulaya Martin Schultz alifahamisha kuwa tatizo la wakimbizi ni tatizo la Ujerumani.

Habari iliochapishwa na jarida la Lefigaro zilifahamisha kuwa waziri Orban alisema kuwa wakimbizi wanoaingia Ulaya wasiwe wawakilishi wa utamaduni fulani na kusema kutiwa wasiwasi na wazawa kuwa idadi ndogo katika ardhi yao.

Soma pia: Angela Merkel, shujaa wa wakimbizi kutoka Syria


Tagi:

Habari Zinazohusiana