TRT TV

 

TELEVISHENI

TRT ni shirika la habari la Uturuki ambalo hutoa habari za ukweli na haki bila kupendelea upande wowote,Habari hufikia sehemu na mikoa mbalimbali na asilimia 90 ya Anatolia nzima,Habari hugusia vipengele mbalimbali kama vile elimu,utamaduni,michezo,documentary,maigizo kwa watu wa umri tofauti.Habari za TRT huchangia kwa kiasi kikubwa kukua na kusambaa kwa elimu ,utamaduni na maendeleo ya taifa zima.Habari huwafikia walengwa ndani ya muda mfupi kabisa.

TRT 1

TRT-1

TRT -1 ni kituo cha televisheni kinachotizamwa sana na familia.Mfumo wa kituo hiki ni kuonyesha vipindi vya elimu,maigizo,utamaduni,muziki,michezo,habari pamoja na burudani.Kituo hicho kimefikia asilima 99 ya Uturuki nzima na vilevile hurushwa kupitia Internet.

TRT HABER

TRT HABER

Hiki ni kituo cha televisheni amabcho hutoa habari zake moja kwa moja kwa lugha ya kiingereza.TRT WORLD hutoa habari halisi na zenye uhakika.

TRT WORLD

TRT WORLD hutoa habari za kisasa,uchambuzi,majadiliano,siasa,michezo,waraka,utamaduni na sanaa.TRT ina uzoefu mkubwa katika kurusha vipindi vyake.Kituo hiki hutoa habari zilizo sahihi bila kubagua wala kuchagua rangi.Pata habari za uhakika kila mahali ulipo.

TRT SPOR

SPOR TRT

kituo cha televesheni cha TRT SPOR kilianza kutangaza michezo mnamo Agosti 2010.Kila aina ya mchezo hutangazwa katika kila kipengele na matukio yote ya kitaifa na kimataifa.Mara nyingi michezo hurushwa moja kwa moja.

TRT AVAZ

TRT AVAZ

Kituo kilichoanza kutangaza Machi 2009 na matangazo hurushwa katika nchi 8  ikiwa ni pamoja na Uzbekistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Turkmenistan, Azerbaijan, Bosnia,Herzegovina, Albania na Uturuki na hutangaza pia katika  eneo la kijiografia  kutoka Mashariki ya Mbali hadi Balkan.Kituo hiki huunganisha lugha na mawazo kati ya Jamhuri ya Kituruki.Neno AVAZ humaanisha sauti katika lugha ya kituruki SES.Hufikia eneo la kijografia la watu milioni 250,mashariki ya kati ,Caucasia, nchi 27 na jamhuri za muhtar 13 kama sauti ya Uturuki.

TRT ÇOCUK

TRT COCUK

Kituo hicho kina dhamira kubwa ya kuelimisha kizazi kipya na vilevile kutoa elimu muhimu kwa watoto jamii nzima,Elimu ya kimwili.kiakili na kitabia na maadili hutolewa kwa watoto wote.Muziki,habari pamoja na michezo kwa ajili ya huonyeshwa kupitia televisheni hiyo.Televisheni hiyo pia husaidia kutoa elimu ya usawa na kuwaelimisha watoto kuwa raia wema na wenye kutimiza majukumu yao katika jamii.Wakati huo huo hutoa burudani kabambe kwa watoto wote.

TRT BELGESEL

TRT BELGESEL

Kituo hicho kinatoa programu za waraka katika historia, jamii, asili, mazingira, michezo, utamaduni, sayansi na teknolojia, Huitangaza  Uturuki ulimwenguni katika lugha tano tofauti ya Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kirusi na Kituruki. Ilianza kutangaza tarehe 17 Oktoba 2009, 

TRT MÜZİK

TRT MUZIK

Programu za ushindani, kumbukumbu za muziki, matamasha, mipango ya jamiii, Programu 10 za mipango ya kuishi hutangazwa kwenye kituo kinachoileta Uturuki pamoja kwa kutumia  muziki wa dunia. Kituo, kilichoanza kutangaza mnamo Novemba 16, 2009, hurusha Muziki wa Kituruki na matangazo ndani na nje ya nchi.

TRT ARAPÇA

TRT-El Arabia,

 ambayo inalenga kuboresha mahusiano ya Uturuki na mataifa ya kiarabu na hutumia lugha ya kawaida kufikisha hisia mbalimbali Iilianza kutangaza mwezi wa Aprili 2010 na hurusha michezo mizuri ya kuigiza, waraka, michezo, muziki, habari, utamaduni-sanaa,  dini na programu za burudani. Kituo hutumia lugha ya Kiarabu, 22 wasemaji wa Kiarabu.Lengo ni kuimarisha mahusiano kati ya Uturuki na jamii ya kiarabu yenye takriban watu milioni 350 wanaotizama televisheni hiyo.

TRT TÜRK

TRT TURK 

Kituo kinachotangaza sana kwa lugha ya Kituruki  ulimwenguni na hupendwa na hutizamwa sana na watu hasa wanaoishi nje ya nchi kwani husaidia kusambaza na kuonyesha mipango inayoendelea nchini,tamaduni,mipango ya utoaji misaada na vilevile kuonyesha vipindi mbalimbali vya huzuni na furaha,

TRT KURDÎ

TRT KURDI

imechangia katika kuleta mahusiano mazuri kati ya  Uturuki na nchi za kimataifa  hasa za kikanda na hutangaza kwa lugha ya kikurdi. TRT Kikurdi hutizamwa na familia nyingi za  Kikurdi  na inalenga kuleta  umoja wa nchi yetu.

ilianza utangazaji Januari 2009.

TRT OKUL

TRT OKUL

ilianza kutanga 2011,na  inachapisha mipango ya  elimu na utamaduni iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Anadolu pamoja na programu za utamaduni.

Programu mbalimbali huonyesha mipango mablimbali ya vijana wa umri tofauti pamoja na tamadunu zao

TRT 3

TRT 3

Matangazo ya Bunge la Uturuki  huonyesha hapa ikishirikiana na TRT spor ,TBMM TV pamoja na TRT 3..