Mashambulizi ya kigaidi Afrika Magharibi

Mashambulizi ya kigaidi

1662044
Mashambulizi ya kigaidi Afrika Magharibi

Watu 2,000, wakiwemo wanajeshi, wameuawa katika mashambulizi 700 tofauti ya kigaidi katika nchi za Afrika Magharibi mwaka jana.

Jean-Claude Kassi Brou, Mwenyekiti wa Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), amesema katika taarifa kwamba magaidi wanaendelea kutishia utulivu wa eneo hilo.

Brou amesisitiza kuwa maswala ya ukosefu wa usalama katika mkoa wa ECOWAS bado ni wasiwasi mkubwa kwa mkoa huo, "Licha ya juhudi kubwa za nchi wanachama wa (ECOWAS), kumekuwa na mashambulizi 700 tofauti ya kigaidi mnamo 2020 na wanajeshi na raia 2,000 waliuawa katika mashambulizi hayo."

Akibainisha kuwa mashambulizi hayo yalitokea zaidi Burkina Faso, Mali, Niger na Nigeria, Brou amesema kuwa idadi ya watu waliohama makazi yao katika maeneo hayo imeongezeka.

Brou ametaka viongozi wafanye juhudi zaidi kumaliza mashambulizi ya kigaidi katika eneo hilo.Habari Zinazohusiana