Mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali

1662112
Mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali

Wanajeshi wengi wamejeruhiwa katika shambulizi ambapo wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali walilengwa na gari lililosheheni bomu.

Kulingana na ripoti kwenye vyombo vya habari vya kitaifa, gari lililosheheni bomu liliwalenga wanajeshi wa Ufaransa katika mkoa wa Timbuktu kama sehemu ya Operesheni Barkhane.

Wakati wanajeshi wengi wakiwa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo, helikopta nyingi zilipelekwa katika mkoa huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema mnamo Juni 10 kwamba atakomesha "Operesheni Barkhane" kama sehemu ya mabadiliko makubwa ya uwepo wa jeshi la nchi yake katika mkoa huo.

Ufaransa ilizindua "Operesheni Barkhane" mnamo Agosti 1, 2014, baada ya operesheni ya kijeshi iitwayo "Serval" huko Mali mwanzoni mwa 2013.

Zaidi ya wanajeshi elfu 5 wa Ufaransa wanafanya kazi katika Operesheni Barkhane, ambayo inagharimu euro milioni 1 kwa siku.Habari Zinazohusiana