Mzozo wa kisiasa nchini Tunisia

Rais wa Tunisia atangaza kuwa tayari kwa mazungumzo ya suluhisho la mzozo wa kisiasa nchini

1656704
Mzozo wa kisiasa nchini Tunisia

Rais wa Tunisia Kais Saied alisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ya suluhisho la mzozo wa kisiasa nchini.

Kulingana na taarifa iliyoandikwa na Ofisi ya Rais wa Tunisia, Rais Saied alimpokea Rais wa Jumuiya ya Wafanyakazi wa Tunisia Nureddin Al-Tabbubi katika Ikulu ya Carthage.

Wakati wa mkutano huo, ambapo mzozo wa kisiasa nchini na njia za suluhisho zilijadiliwa, Saied alisema kwamba yupo tayari kwa mazungumzo ya kisiasa, ingawa alibainisha kwamba hakuna mazungumzo yoyote yatakayoanzishwa na watu wanaoshukiwa kuhusika na rushwa.

Katika nchi ya Tunisia, hali ya utulivu wa kisiasa haikuweza kupatikana kwa muda mrefu, baada ya mapinduzi na uchaguzi wa rais na wabunge uliofanyika Oktoba 2019.

Ajenda ya kisiasa ya nchi hiyo inazungukwa na mzozo kati ya Waziri Mkuu Hisham al-Mashishi na Rais Saied baada ya marekebisho ya baraza la mawaziri yaliyofanyika mnamo Januari 16.

Rais Saied anasema kuwa marekebisho ya baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Mashishi, ambalo lilipokea kura ya imani kutoka kwa bunge, ni kinyume cha katiba. Mvutano kati ya pande hizi mbili huongezeka mara kwa mara nchini humo.Habari Zinazohusiana