Idadi ya vifo yaongezeka Burkina Faso

Idadi ya waliokufa kwenye shambulizi la kigaidi nchini Burkina Faso yaongezeka hadi 160

1652721
Idadi ya vifo yaongezeka Burkina Faso

Idadi ya waliokufa kwenye shambulizi la kigaidi katika kijiji cha kaskazini mwa Burkina Faso imeongezeka hadi 160.

Kulingana na taarifa kutoka vyanzo vya usalama, inahofiwa kuwa idadi ya waliokufa itaongezeka zaidi kutokana na idadi kubwa ya waliojeruhiwa vibaya kwenye shambulizi la kigaidi lililotekelezwa katika kijiji cha Yaghga, mkoa wa Sahel usiku unaounganisha Ijumaa hadi Jumamosi.

Katika nchi ya Burkina Faso ambapo siku tatu za maombolezo ya kitaifa zilitangazwa kuanzia Jumamosi, mashirika mengi ya kimataifa pia yalilaani shambulizi hilo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilaani vikali shambulizi hilo, ambalo alilielezea kuwa "la kudharauliwa", na akataka jamii ya kimataifa iongeze juhudi za uungaji mkono wake kwa mataifa yanayopambana na ugaidi katika eneo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Ulaya, ilielezwa kwamba shambulizi hili "la kinyama" lililaaniwa kwa nguvu zaidi ya hapo awali, na msaada wake kwa vita vya Burkina Faso dhidi ya ugaidi ulirudiwa.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara pia alilaani shambulizi hilo na kutoa ujumbe wa mshikamano na watu wa Burkina Faso.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki pia ilitoa taarifa na kulaani shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana