Mateso dhidi ya wanachama wa FACT nchini Chad

Wanamgambo wa chama cha FACT wadaiwa kuteswa katika gereza walikofungwa nchini Chad

1644827
Mateso dhidi ya wanachama wa FACT nchini Chad

Inadaiwa kuwa karibu wanamgambo 500 ambao walikuwa wanachama wa Chama cha Front for Change and Harmony (FACT) nchini Chad na waliokamatwa walipokuwa wakipambana na vikosi vya usalama nchini Chad, walihifadhiwa katika mazingira yasiyo ya kibinadamu katika gereza la mji mkuu wa N'Djamena.

Wakati wanamgambo 27 ambao walinyimwa chakula na vinywaji wakidaiwa kufariki kwa njaa na kiu, jukwaa la Mkataba wa Kulinda Haki za Binadamu la Chad lilisema kwamba hakuna taarifa kutoka kwa wanachama wengine 5 wa FACT walioshikiliwa katika gereza moja.

Chama cha FACT katika barua yake kwenye Twitter, kilidai kwamba wafungwa wengine walifariki kutokana na mateso.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Ulinzi Daoud Yaya alikanusha madai yaliyoenea kwenye mitandao ya kijamii, akisema kuwa jeshi la Chad kila wakati lilinda hadhi ya wahalifu wa kivita.

Cham cha FACT ambacho kilipinga kuongezwa kwa muda wa Rais wa Chad Idris Debi Itno, kwanza kilianzisha shambulizi kutoka mkoa wa Tibesti, mpakani mwa Libya hadi N'Djamena mnamo Aprili 11, wakati uchaguzi wa rais ulipofanyika.

Baada ya Rais Itno kuuawa mnamo Aprili 19 katika operesheni dhidi ya chama cha FACT kaskazini mwa nchi, mtoto wa Itno Luteni Jenerali Mohammed Idris Debi mwenye umri wa miaka 37 na Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Rais, aliteuliwa kama mkuu wa Baraza la Mpito la Kijeshi mnamo tarehe 20 Aprili.Habari Zinazohusiana