Janga la kipindupindu lasababisha vifo Nigeria

Watu 15 wafariki kwa janga la ugonjwa wa kipindupindu katika jimbo la Kano nchini Nigeria

1638038
Janga la kipindupindu lasababisha vifo Nigeria

Watu 15 wameripotiwa kufariki katika jimbo la Kano nchini Nigeria kutokana na janga la ugonjwa wa kipindupindu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya kitaifa, mkuu wa kijiji cha Koya cha jimbo hilo Sulaiman Muhammad, aliripoti kwamba wengi wa wale waliopoteza maisha walikuwa ni watoto.

Muhammad alibaini kuwa watu 40 pia walichukuliwa na kuwekwa chini ya matibabu.

Kutokana na kushindwa kukidhi mahitaji ya maji safi na ukosefu wa matibabu ya haraka na njia bora nchini Nigeria, kumekuwa na ongezeko la hatari ya magonjwa ya milipuko yanayosababisha vifo.

Magonjwa ya mlipuko na janga kama vile malaria, polio, typhoid na virusi vya nguruwe yamekuwa ya kawaida nchini.Habari Zinazohusiana