Msikiti washambuliwa Nigeria

Watu 40 watekwa nyara baada ya msikiti kushambuliwa na watu wenye silaha nchini Nigeria

1637473
Msikiti washambuliwa Nigeria

Watu 40 walitekwa nyara baada ya shambulizi kutekelezwa kwenye msikiti mmoja katika jimbo la Katsina nchini Nigeria.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya kitaifa, Waislamu walikusanyika katika msikiti huo kutekeleza sala za tahajjud katika wilaya ya Kwata, jimbo la Katsina, ambapo walishambuliwa na watu wenye silaha.

Msemaji wa Polisi wa Katsina, Gambo Ishaka, alitangaza kuwa watu 30 waliokolewa baada ya shambulizi hilo.

Ishaka aliongezea kusema kuwa watu wengine waliotekwa nyara hawajulikani waliko lakini operesheni ilianzishwa ili kuwaokoa.Habari Zinazohusiana