Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia

Watu sita wamepoteza maisha

1637406
Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia

Watu sita, wakiwemo polisi 2, wamefariki katika shambulizi la kujitoa muhanga ambapo kituo cha polisi kililengwa huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Vyombo vya habari vya serikali ya Somalia vimeripoti kuwa shambulizi la kujitoa muhanga lilitekelezwa katika kituo cha polisi katika wilaya ya Waberi ya Mogadishu.

Taarifa iliyoandikwa na polisi imesema, "Watu sita, pamoja na Mkuu wa Polisi Ahmed Bashane na Naibu Kamanda Idara Abdi Basid, wamepoteza maisha katika shambulizi la kujitoa muhanga lililolenga kituo cha polisi katika mkoa wa Waberi."

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, lililolaaniwa na Waziri Mkuu Hüseyin Roble kupitia Twitter.Habari Zinazohusiana