Boti yazama nchini Nigeria

Watu wasiopungua 15 wamefariki kutokana na kuzama kwa boti

1636902
Boti yazama nchini Nigeria

Watu wasiopungua 15 wamefariki kutokana na kuzama kwa boti iliyokuwa na zaidi ya watu 60 katika jimbo la Niger la Nigeria.

Mallam Adam Ahmed, mkuu wa wilaya ya Zumba, amesema mashua iliyokuwa imebeba abiria na bidhaa ilizama katika Mto Shiroro wilayani Zumba katika jimbo la Niger kutokana na kuzidiwa uwezo.

Ahmed ametangaza kwamba watu wasiopungua 15 walifariki katika ajali hiyo, na idadi kubwa ya watu walipotea.

Mkuu wa eneo la Zumba Ahmed alisema kuwa juhudi za kutafuta na kuokoa zinaendelea.Habari Zinazohusiana