Ufaransa yaonywa juu ya kuingilia Chad

Umoja wa Wasomi wa Kiislamu Ulimwenguni waitaka Ufaransa iache kuigilia mambo ya ndani ya Chad

1634721
Ufaransa yaonywa juu ya kuingilia Chad

Umoja wa Wasomi wa Kiislamu Ulimwenguni umetoa wito kwa Ufaransa wa kutoingilia mambo ya ndani ya Chad.

Profesa Dr. Ahmed er-Raysuni, Rais wa Umoja wa Wasomi wa Kiislamu Ulimwengu alitoa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Ali Muhyiddin al-Karadagi, ambapo ilisisitizwa kuwa walikuwa wakifuatilia matukio yanayojiri nchini Chad, hali iliyosababishwa na mapambano ya madaraka na mzozo unaoendelea kati ya Baraza la Mpito la Kijeshi na vyama vya upinzani.

Wakati hali hiyo ikiendelea, taarifa hiyo iliitaka Ufaransa kuondoa jeshi lake kutoka Chad na kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo. Pia ilitoa wito kwa Baraza la Mpito kwamba libadilishe mamlaka ya uongozi kwa amani kupitia uchaguzi huru na wa wazi na kuacha kuwashambulia waandamanaji wa amani.

Baada ya Rais Idris Debi Itno kuuawa mnamo Aprili 19 katika operesheni dhidi ya waasi wa Front for Change and Harmonization (FACT) kaskazini mwa nchi ya Chad, mtoto wa Itno mwenye umri wa miaka 37 ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Rais, Luteni Jenerali Muhammed Idris Debi, aliteuliwa kama mkuu wa Baraza la Jeshi la Mpito mnamo Aprili 20.

Baraza, ambalo lilichukua madaraka nchini Chad, lilitangaza kuwa muda wake wa kazi ulikuwa miezi 18, na bunge pamoja na serikali zilivunjwa. Baraza lilimteua Waziri Mkuu wa zamani Pahimi Padacke Albert kama waziri mkuu wa mpito mnamo Aprili 27.

Watu 6 walifariki na zaidi ya watu 700 walizuiliwa wakati wa maandamano yaliyofanyika Aprili 27 nchini Chad dhidi ya utawala wa Baraza la Jeshi la Mpito.Habari Zinazohusiana