Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Chad

Baraza la Jeshi la Chad lamteua Waziri Mkuu wa serikali ya mpito baada ya kifo cha Rais Idris Debi Itno

1629268
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Chad

Baraza la Mpito la Jeshi la Chad lilimteua Pahimi Padacke Albert kuwa waziri mkuu wa mpito baada ya kifo cha Rais Idris Debi Itno.

Albert, ambaye aliteuliwa kama waziri mkuu wa mpito kwa amri iliyochapishwa na Rais wa Baraza la Jeshi Luteni Jenerali Muhammed İdris Debi, anatakiwa kuunda serikali ndani ya siku 15.

Msemaji wa Jeshi la Chad Azem Bermandoa Agouna alitangaza mnamo Aprili 20 kwamba Itno, mwenye umri wa miaka 68, alishiriki katika operesheni dhidi ya kundi la Chad Change and Unity Front kaskazini mwa nchi na kufariki Aprili 19 baada ya kupigwa risasi kichwani.

Baraza la Jeshi likiongozwa na mtoto wa Itno mwenye umri wa miaka 37 na Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Rais, Luteni Jenerali Muhammed Idris Debi, lilichukua utawala wa nchi mnamo Aprili 20.

Likitangaza kuwa muda wa kuhudumu ni miezi 18, Baraza lilivunja bunge la serikali na kutangaza kuwa serikali ya mpito itaanzishwa.

Upinzani, kwa upande mwingine, unafafanua uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Jeshi kuwa kama "mapinduzi ya kijeshi" na kudai kwamba baraza hilo halina mamlaka ya kuteua waziri mkuu.Habari Zinazohusiana