Hafla ya mazishi ya kiongozi wa Chad

Rais wa Chad Idris Debi Itno aandaliwa hafla ya mazishi na kuzikwa katika mji mkuu wa N'Djamena

1627445
Hafla ya mazishi ya kiongozi wa Chad

Rais Idris Debi Itno, ambaye alifariki katika mapigano na waasi nchini Chad, alizikwa kwa hafla rasmi iliyoandaliwa.

Hafla ya mazishi ilifanyika chini ya hatua  kali za usalama katika mji mkuu wa N'Djamena kwa ajili ya Rais Itno ambapo kulikuwa na ushiriki wa viongozi wengi, mabalozi, viongozi wa serikali na wanajeshi kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Ulaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Jumuiya ya Afrika na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi, Mwakilishi Mkuu wa Jumuiya ya Ulaya na Sera ya Usalama Josep Borrell na mke wa Itno, Hinda Debi walitoa hotuba katika hafla hiyo.

Tshisekedi alisema,

"Jumuiya ya Afrika imepoteza mshirika muhimu. Kuondoka kwa Itno lazima kuunganishe watu wa Chad na Afrika. Tunataka mabadiliko ya kikatiba ya amani, umoja na demokrasia nchini Chad."

Rais wa Ufaransa Macron pia alitoa ujumbe wa mshikamano na msaada, akisema kwamba nchi yake haitaruhusu mtu yeyote kutishia utulivu na usalama wa Chad.

Mazishi ya Itno yalimalizika na akazikwa baada ya sala ya Ijumaa.Habari Zinazohusiana