Moto mkubwa kwenye chuo kikuu cha Cape Town

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Cape Town wahamishwa baada ya moto kuenea na kusababisha uharibifu

1624254
Moto mkubwa kwenye chuo kikuu cha Cape Town
g afrika yangin Cape Town.JPG
g afrika yangin Cape Town.JPG

Wanafunzi elfu 4 walilazimika kuhamishwa baada ya moto kuzuka kwenye Mlima wa Table Mountain hapo jana na kusambaa katika chuo kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.

Moto huo uliozuka kwenye mteremko wa Mlima wa Table Mountain na kuharibu majengo ya chuo kikuu cha Cape Town, haungeweza kudhibitiwa licha ya juhudi za makabiliano kutoka kwa idara ya wazima moto ya jiji.

Moto huo, ambao kwanza uliharibu mgahawa katika Rodes Monument, baadaye ulienea na kusababisha uharibifu wa majengo mengi ya kihistoria ya chuo kikuu.

Shughuli zote za chuo kikuu zilisitishwa na wanafunzi elfu 4 walihamishwa.

Iliripotiwa kuwa wazima moto wengine walijeruhiwa kwa moto huo wakati wa makabiliano na kulazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.Habari Zinazohusiana