Idris Debi Itno ashinda uchaguzi Chad

Rais wa Chad Idris Debi Itno ashinda tena uchaguzi uliofanyika nchini humo

1624800
Idris Debi Itno ashinda uchaguzi Chad

Idris Debi Itno ameshinda uchaguzi wa urais katika nchi ya Chad iliyoko Afrika ya Kati.

Kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Kitaifa, Rais wa sasa Idris Debi Itno, ambaye alikuwa mgombea kwa mara ya 6, alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 79.32 ya kura.

Pahimi Padacke Albert alipata asilimia 10.32 na mgombea pekee wa kike Beassemda Lydie alipata asilimia 3.16, wakati wagombea wengine 7 wakipata chini ya asilimia 2 ya kura.

Nchi ya Chad, ambayo ina takribian wapiga kura milioni 7 na elfu 300, kiwango cha ushiriki katika uchaguzi uliofanyika Aprili 11 kilikuwa asilimia 64.81.

Rais Itno, ambaye ametawala nchi kwa zaidi ya miaka 30, alifungua njia ya kutawala kwa mihula miwili zaidi, kila moja kwa miaka 6 baada ya kumalizika kwa kipindi chake mwaka huu, kutokana na marekebisho ya Katiba yaliyofanyika mwaka 2018.

Baadhi ya viongozi wa upinzani walitoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi huo.

Wakati upinzani ulimshtaki Itno, ambaye alitawala Chad kwa zaidi ya miaka 30 kwa madai ya kujaribu kuanzisha uongozi wa kifalme nchini, Itno alitangaza kuwa alikuwa mgombea tena kwa sababu ya imani ya watu kwake.Habari Zinazohusiana