Idadi ya vifo yaongezeka Chad

Idadi ya waliopoteza maisha imeongezeka hadi 100

1624227
Idadi ya vifo yaongezeka Chad

Idadi ya waliopoteza maisha imeongezeka hadi 100 katika mapigano kati ya makabila kusini mwa Chad.

 idadi ya watu waliopoteza maisha katika mapigano kati ya Waarabu kwa upande mmoja, na makabila ya Dagal na Kibet kwa upande mwingine, imeongezeka hadi 100 Katika vijiji vya Sihep na Ambarit katika mkoa wa Salamat.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (CNDH) nchini humo iliitaka serikali kutangaza hali ya dharura katika mkoa wa Salamat, ikisisitiza hitaji la kuwapokonya watu silaha.

Gavana wa Salamat Jenerali Yambaye Massyra Abdel alisema wiki iliyopita kwamba nyumba kadhaa zilichomwa moto wakati wa mapigano, na vikosi vya usalama vilipelekwa katika eneo.Habari Zinazohusiana