Uchaguzi mkuu wafanyika Chad

Wananchi wa Chad wajitokeza kupiga kura ili kumchagua rais mpya kwenye uchaguzi mkuu

1619216
Uchaguzi mkuu wafanyika Chad

Nchi ya Chad iliyoko Afrika ya Kati, imefanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kumchagua rais mpya.

Mchakato wa upigaji kura ulioanza hapo jana mwendo wa saa 06.00 kwa saa za ndani ya nchi, uliendelea hadi saa 19.00.

Katika nchi hiyo ambayo kuna wapigaji kura milioni 7 na laki 3 waliojiandikisha kulingana na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi, Mahakama Kuu ya Chad ilikubali maombi ya wagombea 10 katika uchaguzi wa urais, ingawa  7 kati yao walitangaza kwamba watashiriki katika uchaguzi huo.

Rais Idris Debi Itno, ambaye alipiga kura yake asubuhi na mapema, alitoa wito kwa umma kutimiza majukumu yao ya kiraia.

Rais wa Chad Idris Debi Itno amekuwa akitawala nchi hiyo tangu mwaka 1990 chama chake cha Harakati ya Ukombozi wa Kitaifa kilipoingia madarakani.

Mbali na Rais Idris Debi Itno, Roumadoumngar Nialbe Felix, Pahimi Padacket Albert, Yombombe Madjitoloum Theophile, Beassoumda Lydie, Alladoum Baltazar Djarma na Mbaimon Guedmbaye Brice pia wameshiriki kama wagombea katika uchaguzi huo.Habari Zinazohusiana