Rais wa zamani wa Madagascar afariki dunia

Didier Ratsiraka, Rais wa zamani wa Madagascar afariki hospitalini akiwa na umri wa miaka 84

1610172
Rais wa zamani wa Madagascar afariki dunia

Didier Ratsiraka, Rais wa zamani wa Madagascar ambayo ni nchi ya kisiwa katika kanda ya Afrika Mashariki, ameaga dunia.

Familia yake ilitangaza kuwa Ratsiraka mwenye umri wa miaka 84, alifariki hapo jana mida ya asubuhi katika hospitali ya kijeshi alikokuwa akitibiwa homa ya mafua.

Madaktari walitangaza kuwa vipimo vya afya vya rais huyo wa zamani vilionyesha kwamba hakuwa na virusi vya corona (Covid-19).

Didier Ratsiraka, ambaye pia alitambulika kwa jina la utani la "Admiral" kutokana na asili ya kijeshi, aliwahi kuwa rais wa awamu mbili za kati ya 1975-1993 na 1997-2002.Habari Zinazohusiana