Mapigano yazuka Nigeria: 20 wafariki

Watu 20 wafariki kwenye mapigano kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama

1608764
Mapigano yazuka Nigeria: 20 wafariki

Watu 20 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mapigano yaliyozuka kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama vya mitaa katika jimbo la Niger nchini Nigeria.

Diwani wa Mariga katika jimbo la Niger, Ibrahim Ilyasu alisema kuwa watu wenye silaha walipigana na vikosi vya usalama vya mitaa katika kijiji cha Kotonkoro mkoani Mariga.

Ilyasu alibaini kuwa wanajeshi walitumwa kwenye mkoa, baada ya mzozo huo kusababisha vifo vya maafisa 20 wa vikosi vya usalama ambapo miili yao ilipatikana katika eneo hilo.

Ilyasu aliongezea kusema kuwa wanajeshi waliweza kudhibiti hali ya usalama katika mkoa huo.Habari Zinazohusiana