Kamanda wa vikosi vya Haftar auawa Libya

Kiongozi mmoja wa wanamgambo wa vikosi vya Haftar afariki kwenye shambulizi la mauaji Benghazi Libya

1608548
Kamanda wa vikosi vya Haftar auawa Libya

Mahmoud al-Warfalli, kamanda wa wanamgambo wa Haftar, ambaye agizo la kukamatwa kwake lilitolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) nchini Libya kwa uhalifu wa vita, amepoteza maisha kutokana na shambulizi la mauaji lililomkumba Benghazi.

Kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya Libya, Warfalli alishambuliwa kwa bunduki karibu na Chuo Kikuu cha Matibabu cha Kiarabu katika mji wa Benghazi.

Ilitangazwa kwamba Warrfalli alifariki kutokana na shambulizi hilo.

ICC ilitoa agizo la kukamatwa kwa Warfalli mnamo 2017 kwa madai kwamba "alitekeleza uhalifu wa kivita, akawaua watu 33 katika maeneo tofauti ya Benghazi na kuwanyonga watu 6 wasiokuwa na hatia."

Umoja wa Ulaya pia ulimjumuisha Warfalli na mtu mwingine kwenye orodha ya vikwazo mnamo Septemba 2020, na mashirika matatu kwa madai kwamba yalikiuka haki za kibinadamu nchini Libya.

Picha nyingi za mauaji ya umati na harakati za ukandamizaji dhidi ya raia ambazo Warfalli na wanamgambo wake walikuwa wamefanya hapo awali zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.Habari Zinazohusiana