Shambulizi mjini Mogadishu

Watu 3 walipoteza maisha katika shambulizi Mogadishu

1608348
Shambulizi mjini Mogadishu

Watu 3 walipoteza maisha katika shambulizi la mzinga wa mortar  lililolenga Umoja wa Mataifa (UN) na majengo ya Umoja wa Afrika huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Afisa wa Mkoa wa Dharkinley, Abdi Yusuf, alitangaza kwamba Kambi ya Halane, ambapo kuna Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zimeshambuliwa na makombora.

Yusuf amesema kuwa raia wasiopungua 3 wamepoteza maisha na watu 5 wamejeruhiwa kutokana na makombora kugonga nyumba karibu na kambi.

Shirika la kigaidi Al Shabaab limedai kuhusika na shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana