Nigeria yaboresha chanjo mbili za Covid-19

Chanjo mbili za ndani dhidi ya virusi vya corona (Covid-19) zaboreshwa nchini Nigeria

1607741
Nigeria yaboresha chanjo mbili za Covid-19

Chanjo mbili za ndani dhidi ya virusi vya corona (Covid-19) zimeboreshwa katika nchi ya Nigeria iliyoko Afrika Magharibi.

Katibu wa Serikali ya Nigeria na Mkuu wa Kupambana na Covid-19 Boss Mustapha, alisema katika taarifa kwamba wanasayansi nchini humo wameboresha chanjo mbili za ndani dhidi ya Covid-19.

Akibainisha kuwa majaribio ya kliniki ya chanjo hizo zilizoboreshwa bado yanaendelea, Mustapha alisema,

"Chanjo zitatumika baada ya majaribio ya kliniki kukamilika na kuthibitishwa. Hii italeta mtazamo mpya katika mafanikio ya kisayansi na kuongeza ari na nguvu ya tasnia ya matibabu nchini."

Mustapha pia alitoa wito wa kuunga mkono taasisi husika ili kuwatia moyo na kuwahamasisha watafiti wa kisayansi nchini.

Nigeria hapo awali ilikuwa imepokea dozi milioni 4 na elfu 224 za chanjo ya AstraZeneca chini ya Mpango wa Ufikiaji wa Chanjo ya Covid-19 (COVAX).Habari Zinazohusiana